Select Page

Januari tarehe 11 ninaanza tena ku “up-load” masomo kwenye channel yetu ya youtube. Tumeamua kubadilisha mfumu wetu wa kazi na kuanzia sasa video zetu zote zinapatikana moja kwa moja kwenye Youtube na siyo hapa kwenye site yetu.

Tarehe 11 Januari 2021 video ya kwanza itakuwa live! Mimi binafsi ninajisikia sana juu ya somo hili ninalolileta kwa sababu ni ya kitabu cha Bibila, ni Injili ya Marko.

Wiki ya kwanza nitatoa video mbili, ya kwanza ni kutambulisha somo yenyewe na katika ya pili tunaanza kusoma maandiko yenyewe. Kipindi cha pili tunaangalia Marko sura ya kwanza na mstari wa kwanza. Ndiyo masomo yako youtube lakini haina maana kwamba tunalipua utapata masomo mazuri kabisa kama ulivyozoea kupata kupitia site yetu. Nakukaribisha sana